Mafunzo yanatolewa kwa njia gani?

Mafunzo yanatolewa kwa mfumo wa videos ambazo zipo tayari zote kwenye channel ya telegram hivyo ukiunganishwa unapata access ya videos za mafunzo, program na resources zingine za kujifunzia, na kukuwezesha kujifunza kwa muda wako huku sisi tunakupatia usaidizi mpaka unamaster hatua kwa hatua.

 

Mnatoa Vyeti?

Hapana. Hatutoi vyeti mafunzo ni kwaajili ya kupata ujuzi wa ziada.

 

Ofisi zenu zipo wapi?

Tunapatikana Bwanga Mkabala na (Round About) Barabara iendayo Wilaya ya Chato mafunzo yanatolewa ofisini kwa watu walioko karibu,  kwa walioko mbali  ni kwa njia ya mtandao tu (yaani Online).

 

Mafunzo ni ana kwa ana?

Ndio mafunzo ni ana kwa ana kwa watu walioko karibu na ofisi zetu, kwa walioko mbali na Ofisi,  Mafunzo sio ana kwa ana ni online pekee kwa mfumo wa videos.

 

Nataka kujiunga na mafunzo ila sina programu/software

Ukijiunga na mafunzo unapatiwa software na kila kitu unahitajika uwe na kompyuta tu.

 

Nahitajika niwe na nini ili nijiunge na mafunzo?

Unahitajika uwe na kompyuta (Laptop au desktop), ili uweze kusoma kozi za mafunzo ya Computer, video editing, website design, motion design, graphics design n.k

 

Nikijiunga na mafunzo naweza kudownload na kuwa nayo offline?

Ndio. Unaweza kudownload ukasoma ukiwa offline kwa muda wako utakaojipangia kusoma.

 

Nitaamini vipi nikituma pesa yangu kuwa sitapeliwi?

Hatupo hapa kuwatapeli watu, kitu cha kwanza hakikisha unasoma taarifa zote muhimu kwenye website yetu na mitandao yetu ya kijamaii na ukiona kuna kitu bado kinakupa wasiwasi wasiliana na sisi kupitia whatsapp ili upate ufafanuzi zaidi kisha ndo utume pesa.

 

Itanichukua muda gani kujua Kozi ya Computer, Internet,  Graphics design/Video editing n.k ?

Inategemea na wepesi wa kichwa chako na idadi ya kozi utakazo chagua kusoma kama ni kozi nyingi  inaweza kuchukua mwezi mmoja na nusu hadi miezi sita kumaster kozi husika ulizochagua.

 

Naweza kulipia nusu nusu Ada ya mafunzo?

Hapana Ada inalipwa yote kwa awamu moja tu.

 

Sina telegram najifunza vipi?

Telegram ni application inayosapoti kwenye kompyuta na simu kama ilivyo whatsapp ingia google au google playstore kisha download na ujiunge

 

Nikikwama napata usaidizi?

Wakati wa mafunzo popote unapopata ugumu unawasiliana na mwalimu anakusaidia papohapo.

 

Mimi sijui chochote kuhusu Computer/ Mtandao wa Internet/video editing/graphics design/motion design na mafunzo mengine, mafunzo haya yatanifaa?

Ndio yatakufa mafunzo haya yameanzia level ya chini kabisa kwa mtu ambae hajui chochote hadi level ya juu kabisa ambapo utafanya projects zako.

 

Sijui chochote kuhusu Computer, Internet, graphics design unanishauri nianze na programu ipi?

Kama haujawahi kabisa kujifunza programu yoyote  Anza na Mafunzo ya Computer then utafuatia na mafunzo ya design nakushauri introduction to Computer baada ya hapo fuatia  na adobe Illustrator au Adobe photoshop ndio programu rahisi kwa graphics designers na zingine zitafuata kulingana na unataka uwe katika sehemu ipi..

Nataka nisome video editing nisome software ipi?

Soma Adobe premiere pro ni software nzuri zaidi kwa video editing.