KUHUSU  COSTEIJEN TECHNOLOGY.

COSTEIJEN TECHNOLOGY ilianzishwa mwaka 2022 na Costeijen  John ambae alikuwa na lengo la kuhitaji watu wajifunze mambo ya kidigitali  kwa kutumia lugha ya Kiswahili na kiingereza  kuhusiana na mambo mbalimbali yanayohusu Computer,  softwares za kompyuta pamoja na simu namna ya kuzitumia kwaajili ya kuleta matokeo chanya katika nyanja mbalimbali.

Kwasababu aliamini kujifunza kwa kutumia lugha yako mama kunafungua nafasi kwa watu wengi zaidi kuweza kuelewa kwa urahisi kitu kinachofundishwa ukifananisha na kujifunza kwa lugha za kigeni ambazo inapelekea kukariri zaidi na kupata uvivu wa kusoma kinachofundishwa.

Wakati inaanzishwa ilikuwa na kozi Mbili  tu ambayo ilikuwa Mafunzo ya Computer na Mtandao wa INTERNET ), Lakini baada ya miaka Kadhaa tulifikia lengo letu na kuwa na kozi takribani 30+ katika platform tofauti tofauti.

COSTEIJEN TECHNOLOGY  inajihusisha na kutoa mafunzo ya kompyuta mtandaoni kwa lugha ya kiswahili, inatoa mafunzo ya kozi kama vile Graphics design, Video editing, motion design, microsoft office na Website design lakini pia kufanya kazi mbalimbali za Graphics design, Video Editing, Website design na motion design kwaajili ya watu binafsi, makampuni na taasisi mbalimbali.